Wanyama kulipwa milioni 8 kila wiki kwa miaka mitano na club brugge

wanyama club brugge
wanyama club brugge
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Spurs na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama amepewa mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya £65,000- kwa wiki na Club Bruges wakati anapokaribia kukamilisha uhamisho. (Scottish Sun)

Inter Milan imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu kiungo wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, na wanataka kukamilisha mkataba wa mkopo katika siku tatu zijazo. (Mirror).

Barcelona imewasilisha ombi jipya kwa mshambuliaji wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain na wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka 27, linalojumuisha "fedha zaidi na wachezaji zaidi". (Telefoot )

Tottenham inahofia itampoteza mchezaji wa kiungo cha kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, fkwa kitita kidogo cha £30m kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Star)

Kalbu ya Fiorentina katika ligi ya Serie A inajitayarisha kuwasilisha ombi kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Fred, mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato)

Norwich itamfukuzia kipa wa Stoke na timu ya taifa ya England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari na iwapo thamani yake itashuka. (Sun)

Bordeaux inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na Misri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, kwenda Ligue 1 kwa mkopo. (Foot Mercato)

Leeds inatarajiwa kuanza mara moja mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati Kalvin Phillips kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo wa miaka 23 anataka kulipwa £40,000 kwa wiki ili kuendelea kusalia Elland Road. (Football Insider)

Aliyekuwa beki kamili wa Chelsea Filipe Luis, mwenye umri wa miaka 34, amekataa ombi la Manchester City, Lyon na Borussia Dortmund msimu huu wa joto kabla ya kujiunga na Flamengo kutoka nchini anakotoka Brazil. (Globo Esporte)

Aliyekuwa beki wa kulia wa Leicester Danny Simpson, mwenye umri wa miaka 32, anafanya mazungumzo na klabu ya Ligue 1 - Amiens kuhusu uhamisho. (Sun)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemkaribisha mchezaji wa kiungo cha kati wa Exeter Ben Chrisene kufanya mazoezi na klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka timu ya vijana wa timu ya taifa England alifanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza mwezi huu. (Sun)

-BBC