Harmonize na Konde Gang ni biashara za lebo ya Wcb. Balaa kubwa kwa Kondeboy

Harm__1566915846_83167
Harm__1566915846_83167
Baada ya mojawapo ya mameneja wa lebo kubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati WCB Sallam kutangaza kuwa msanii Harmonize yupo katika mikakati ya kutemana na lebo hiyo, Babu Tale sasa anasema kuwa swala la Harmonize kutoka katika WCB haiwapigi mshipa katu.

https://www.instagram.com/p/B1ik6rlHzWh/

Soma hii hapa:

Kwa mujibu wa uongozi wa lebo ya Wasafi, mkali wa Never give Up alidondosha barua akitaka kubanduka rasmi. Balaa nzito inaonekana kutokea baada ya taarifa kuwa huenda staa huyo akawa amesaini mkataba wa miaka 15.Hii ina maana kuwa kwa nafsi yake hayupo Wasafi ila anabanwa na mkataba aliousaini. Kulingana na Babu Tale, mkataba wao na msanii huyu unadokeza kuwa chochote Harmonize atakachofanya kinachohusisha burudani au muziki ni biashara yao.

Soma hapa hadithi nyingine:

 Kwa kauli hiyo, endapo Konde Boy atasaini msanii mpya katika kikundi atakachokwenda kuanzisha Konde Gang ,WCB  itakuwa inatengeneza hela kupitia kikundi hicho.

"Sioni ubaya wa kuweka familia ndani ya familia.mkataba wetu sisi unamface Harmonize. Ukimzungumia Harmonize ile ni biashara yetu kulingana na mkataba wetu. Akiweka chochote kinachohusiana na muziki nacho kinaingia WCB. Anavyotanuka huko kwingine bado kuna mrija unaingia WCB." Babu Tale

Soma hapa: