Mariga kuania kiti cha Kibra kwa Jubilee

MARIGA
MARIGA
Nyota wa kabumbu Macdonald Mariga ni miongoni mwa wanaowania tikiti ya chama cha Jubilee katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju alitoa orodha ya wagombeaji watano wanaomezea mate kiti hicho kwa tiketi ya Jubilee. Watano hao ni Morris Peter Kinyanjui, Walter Trenk, Said Ibrahim na Doreen Wasike.

Uchaguzi mdogo wa Kibra umepangiwa kufanyika Novemba tarehe 7.  Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Ken Okoth Julai 26 baada ya kuugua saratani kwa mugda mrefu. Kinyanjui alikuwa mgombeaji wa Jubilee katika kiti hicho mwaka 2017 naye Ibrahim aliwania kitihi cho kwa tikti ya TNA mwaka 2013.

Trenk, ambaye aliwania kiti cha useneta wa Nairobi kwa kiteti ya UDP, alipeleka tume ya Uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) mahakamani kwa kudinda kuchukuwa stakabadhi zake za uteuzi katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Wasike alikuwa amechaguliwa mgombeaji wa Jubilee katika uchaguzi wa mwaka 2017.