Inspekta Mwala anusurika kichapo cha umati. Agonga na kuua mtu papo kwa hapo

Screenshot_from_2017-06-24_11_03_21
Screenshot_from_2017-06-24_11_03_21
Muigizaji Davies Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala amehusika na kugonga na kuua mpita njia papo kwa hapo katika barabara ya Kaloleni- Mazeras kaunti ya Kilifi.

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Patrick Okeri amesema kuwa Mwala alikuwa ameendesha gari aina ya Toyota Axio usiku wa jumatatu alipotatizika barabarani na kumgonga Samuel Mwaki.

Soma hapa:

 Muigizaji huyu alizuliwa kwa muda katika kituo cha Polisi cha Rabai baadaye kuachiliwa kwa dhamana ya kitita cha pesa.
"Tulimwachilia kwa sababu familia ilichukua muda mrefu kuandikisha ripoti katika kituo cha polisi. Tunasubiri kuona iwapo kutakuwa na makubaliano na familia ya mwendazake kabla tuchukue hatua," alisema Okeri

Taarifa zinaonyesha kuwa Mwala alikuwa anasafiri kutoka hafla ya mazishi kuelekea Mombasa alipohusika katika ajali hii.

Maafisa wa polisi walifika ghafla kumkinga na wananchi waliotaka kumvuruga baada ya kisa hicho.

Soma hapa:

"Sina la kusema. Polisi wanajua kilichofanyika,"Mwala alibana kueleza matukio alipopigiwa simu na gazeti la Star.

Mwili wa mwendazake umekimbizwa Coast General Hospital huku gari ya Mwala ikisalia katika kituo cha Polisi cha Rabai.