Aliyekuwa mchezaji wa Harambee stars McDonald Mariga amepata pigo katika jitihada zake za kutaka kuwa mbunge wa Kibra baada ya kugundulika kwamba jina lake halimo katika sajili ya wapiga kura ya IEBC . Afisa wa IEBC Beatrice Muli amemwambia Mariga kutafuta usaidizi kutoka kwa bodi ya kusuluhisha mizozo ya IEBC .
" Tumefutilia mbali uteuzi wa Mariga’ amesema afisa huyo .Hata hivyo stakabadhi nyingine alizowasilisha kwa IEBC zipo sawa . Mbunge wa Lang'ata Nixon Korir na aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale walijaribu kumshawishi kamishna wa IEBC kutumia muda wake wa kutosha kuliangalia jina la Mariga katika sajili .Mariga ana siku saba kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumfungia nje ya uchaguzi huo . Chama cha Jubilee awali jumanne kilikuwa kimemkabidhi Mariga cheti cha uteuzi .
"Kazi ianze sasa..imebaki kwenda kwa mafans. Mariga alisema wakati alipokabidhiwa cheti cha Jubilee
Walioandamana naye ni Didmas Barasa (Kimilili), Caleb Kositany (Soy), na Gladys Shollei (mwakilishi wa akina mama wa Uasin Gishu).