Daah! Fred Omondi afunguka na kusema ameokoka

Katika mahojiano kati ya Fred Omondi na Radio Jambo, Fred Omondi, nduguye Eric Omondi, alifuguka na kusema kuwa ameokoka na anataka kuanza kuimba nyimbo za injili.

Zaidi ya hayo, alisisitiza na kusema kuwa, hata kama biashara zake nyingi ni za kuuza pombe, haoni kama hicho ni kikwazo cha kumfanya asiimbe nyimbo za injili na Mungu amemwita aimbe nyimbo za injili.

Aidha, Fred alisema kuwa hajali mambo ama midomo ya watu watakao mkashifu kwa kuimba nyimbo za injili ilhali yeye ni muuzaji wa pombe kwani anajisimamia kurekodi mziki huu na hakuna anayempa usaidizi wa hela kurekodi nyimbo zake.

Vile vile, Fred Omondi, baba ya mtoto mmoja wa kike, alitujuza, kuwa kwa sasa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na binti yeyote na kuwa, amerudi kwenye ''market'' ya kutafuta na kupata mpenzi.

Wacha tungoje kwa hamu nyimbo ambazo Fred Omondi atatubariki nazo.

&t=54s