Vurugu baada ya mtoto mwenye Autism kuzama Naivasha

autism child
autism child

Maskini wa Mungu! Watoto wasiojiweza walikuwa wameenda kwenye ziara ya shule, na walipokuwa wakicheza karibu na mto Malewa, mmoja wao akateleza na kusombwa na maji.

Familia ya Bwana na Bi Paul Macharia Gichimu wanaishtaki shule ya Little Hands Academy iliyo karibu na mji wa Naivasha kwa uvivu wa kutowaangalia watoto hawa wasiojiweza baada ya mtoto Dalton Gichimu, kusombwa na maji.

Mwili wa mtoto huyu ulipatikana na polisi pamoja na wanakijiji ukielea kwenye mto Malewa jumatatu jioni. Wazazi wa mtoto huyu Dalton, walikuwa na simanzi na huzuni kwani hawakuwa wanaamini yaliyotendeka.

Jamaa na marafiki walikuwa na huzuni pia  na kusema mengi huku wakisisitiza kuwa, shule ndiyo iliyokuwa na makosa kwa kutowaangalia watoto hawa wasiojiweza mpaka mmoja wao akasombwa na maji.

Paul Macharia Gichimu, baba ya mtoto huyu alishangaa mbona shule hii ilichagua kuwapeleka watoto hawa mtaaa huo wakijua fika kwamba mtaa huo, huwa ni mtaa hatari sana si kwa watoto pekee bali pia kwa watu wazima. Vile vile,alisema kuwa wazazi hawakuwa wamejuzwa kuwa watasafiri na kuenda kwenye kambi hiyo.

“The area has a very steep cliff that drops into the river and it’s even unsafe for adults. I wonder why the management settled for the location in the first place,” Paul Macharia alisema.

Zaidi ya hayo, baba ya mtoto huyu alisema kua mtoto wao alikuwa anahitaji kutunzwa kwa njia spesheli na ndio maana yeye na mke wake, waliamua kumpeleka kwenye shule hiyo. Kwa huzuni tele, Paul Macharia alisema kuwa iliwachukua saa moja walimu kujua kuwa, kuna mtoto aliyekuwa amepotea na walipompata walipata mwili wake ukielea majini.

Baba huyu mwenye watoto watatu alisema kuwa wakati huu ndio uliokuwa wakati wa uchungu zaidi maishani mwake na kusema kuwa, alikuwa na matumaini mengi sana kwa mtoto wake Dalton na ni ombi lake mzazi wowote asipatwe na janga kama hilo.

“Despite suffering from autism Dalton had special talent and was a joy to the family and my prayers is that no other parent will undergo the pain that we are currently undergoing,” alisema.

OCPD wa Naivasha, Bwana Samuel Waweru alithibitisha kitendo kilichofanyika na kusema kuwa, iwapo watapata ushuhuda wa kutosha na kuona kuwa ni ukweli shule hii ilikuwa na negligence, basi hatua kali itachukuliwa.

“We have embarked on our own investigations to determine if there was negligence on the part of the school and if there was any definitely the law will take its course,” alisema

Mwalimu wa shule hii ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa bado wanashangaa kwani hakuna kitendo chochote kama hichi ambacho kimewahi fanyika shuleni humo.

Vilevile, tumeamua kuomboleza na familia hii na kisa hiki ni kisa ambacho kimetutikisa sote kwani hakuna mwalimu ambaye aligundua kuwa mtoto huyo hakuwa na wenzake.

“We have decided to mourn in silence with the parents and it’s an incident that has left us shaken as none of the teachers realised that the minor had slipped from the other students,” mwalimu alisema.