Watoto ni baraka! Mastaa waliobarikiwa watoto mwaka huu

Watoto ni baraka kubwa sana kwa binadamu yeyote yule na kawaida, wawili wanapofunga ndoa, wao huomba watunukiwe baraka ya watoto.

Ni bayana kuwa mwaka wa 2019 umekuwa na baraka tele kwa  'maceleb' wa humu nchini kwa kupata wana. Tumekuandalia orodha ya ''mastaa'' waliobarikiwa na watoto na wanaotarajia watoto hivi karibuni.

1.Kate Actress  

  

Kwa muda sasa, wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakidokeza kuwa muigizaji Kate almaarufu, Kate Actress ana uja uzito.

Mrembo huyo alikuwa amekana kuwa mja mzito akidai kwamba tumbo lake lilikuwa limefura tu, na wengi wakamuamini huku wakidhani ni umbea tu.

Hata hivyo, miezi kadhaa baadaye aliamua kutangaza habari njema huku akifichua kuwa anatarajia mwana mwingine miaka 13 baada ya kuzaa mtoto wake wa kwanza.

Kate alijaliwa mwana wake wa kwanza akiwa msichana mdogo na anafichua kuwa hakujua jinsi jambo hilo lingemuathiri. Hata hivyo, ana furaha zaidi kuwa mumewe Phil alisalia naye ikijulikana kuwa mashabiki wao walikuwa wanawasukuma zaidi kupata mtoto pamoja.

Aliandika,

@phil_director Thank you for your patience, I had no idea how much being a teenage mum affected me. You gave me assurance that you would never leave us, you have held my hand all through, spoilt me silly, I am indeed blessed. We thank God, This is such an honor 🙏🏿❤️

2.Diana Marua 

Bahati na mkewe Diana Marua walimkaribisha mtoto wao wa pili mwaka huu.

Wapenzi hawa walimuita mtoto wao Majesty na ni wazi kuwa mtoto huyu ni mfalme kwani alipokelewa kwa mbwembwe zisizo kifani.

3.Kambua

 Kambua na mume wake walipata zawadi yao mwaka huu baada ya kungoja mtoto kwa miaka mingi.
Wapenzi hawa walipopata mtoto wao wa kwanza, walipongezwa sana kwani mashabiki wao wengi walikuwa wamesubiri sana kuona mtoto wake Kambua.

4. kabi wa Jesus
Binti Kabi wa Jesus alibarikiwa mtoto mwaka huu na ni bayana kuwa, alijawa na furaha kwani mtoto ni baraka.
5.Tanasha Donah.
Binti Tanasha Donah ambaye ni kidosho kutoka mumu humu kenya , ana uja uzito wa Staa wa bongo Diamond Platnumz .
Barafu huyo wa Diamond anatarajia  kujifungua mtoto wa kiume kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Bila shaka, mwaka huu umekuwa wa baraka Tele kwa wasanii wetu.