Harmonize ni msanii namba moja kwa sasa Tanzania – Q Chief

69566746_1334649576659335_2229789568296015681_n
69566746_1334649576659335_2229789568296015681_n
Staa mkongwe wa Tanzania Q Chief sasa anahoji kuwa Harmonize kwa wakati huu ndiye staa mkubwa Tanzania.

Katika mahojiano, Q Chief ambaye anaonekana karibu sana na Konde Boy amezungumza mengi kuhusu maisha yake ya muziki.

Aidha, staa huyu amesema kuwa kutoka kwa Harmonize WCB ni ishara ya mwana kukua.

"Kuna kipindi mtoto analelewa na baba. Kikubwa unachotakiwa kujua ni kumheshimu baba. Harmonize sijawahi sikia akimzungumzia Diamond vibaya..."

Soma hadithi nyingine:

Q Chief amesema kuwa yupo kwenye usimamizi wa  Konde Gang ya Harmonize.

"Konde Gang ni lebo yangu. Nyuma ya hizo projects yupo mwenyezi Mungu..."

Kama mwandani wa Harmonize, staa huyu amekana taarifa za uhasama kati ya Diamond na msanii aliyemtengeza.

"Tangu hizi issues zianze, Harmonize sijawahi sikia akizungumza kitu negative kumhusu Diamond..."

"Ni kwa sababu anaheshimu. Watu wanatakiwa kuona vile ana akili kubwa."

Kuhusu iwapo anajua kilichofanyika kupelekea Harmonize kuitema WCB, Q Chief amesema kuwa ana ufahamu wowote.

Soma hadithi nyingine:

'Nyuma ya pazia hatujui ni nini kinaendelea. Ukaribu wangu na Harmonize haunipi kujua kabisa kinachofanyika."

Aidha, amewaonya watu wanaomchamba staa huyu katika mitandao ya kijamii.

"Inaniuma sana mtu anaposema atakwama. Kwa nini mtu hafikirii kuwa Mungu atamsaidia apae juu."

"Comment mbaya zinamjenga na hata comment nzuri zinamfanya awe imara zaidi."

"At least naona furaha iliyopotea miaka mingi. Nawashukuru sana waandishi wa habari, nimshukuru Harmonize, Diamond kwa kuipeleka game juu."

"Lakini sisemi kuwa msanii wangu Harmonize hana mchango wowote. Kama unavyoona sasa,yeye ndiye msanii namba moja Tanzania."