Maelezo A-Z kuhusu talaka ya Sarah na Cohen, Sarah alimnyima Cohen tendo la ndoa

unnamed
unnamed
Vita, mali na kunyimwa tendo la ndoa vilikuwa baadhi ya vijimambo vilivyochangia kuvurugika kwa ndoa ya Cohen na Sarah.

Stakabadhi za kortini zinaonyesha wazi kuwa ndoa ya wawili hawa ilijawa na vitendo vikubwa vya unyama.

Soma hadithi nyingine;

Kwa mujibu wa ripoti hii, taswira ya ndoa iliyosheheni songombingo, ugomvi unatokea na kutoa ishara kuwa hakuna kingesetiri ndoa hii.

Inadaiwa kuwa Cohen alifanya juhudi zote kumfurusha Sarah katika nyumba yao iliyopo Lower Kabete.

Cohen alipotea Julai na baadaye mwili wake kupatikana katika tanki iliyofukiwa ardhini Septemba 13.

Mjane Wairimu, 52,  kwa sasa amezuiliwa katika jela ya mahabusu ya wanawake Lang'ata.

Sarah anatakiwa kuwasili mahakamani Jumanne kujibu mashtaka ya mauaji.

Cohen, 71, ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha kesi kortini kuvunja ndoa yao Januari 21.

Soma hadithi nyingine;

Alisema kuwa Sarah alikuwa anamnyima tendo la ndoa mnamo mwaka wa 2014.

Aliongeza kuwa walikuwa wanalala vyumba tofauti na alikuwa akitayarisha chakula chake.

Mwezi wa Februari 25, Cohen alibatilisha misingi ya kuomba talaka kwa misingi ya unyama na vita kutoka kwa Sarah.