Kweli Pesa ni maua! Tazama Diamond alivyosherehekea siku yake ya kuzaliwa

Mwanamziki bomba sana wa nyimbo za Bongo, Diamond Platnumz alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa njia ya kipekee sana.

Staa huyu amefikisha umri 30 ya maisha yake na huu mwaka, Jalali aliweza kumjalia mema kweli kwani, jamaa huyu aliweza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na kitoto chake kichanga kilichozaliwa siku hiyo.

Nafikiri sote tulidhani kuwa binti Tanasha alikuwa tayari ashajifungua mtoto wake na Diamond lakini ni kama kwamba kitoto hiki kilikuwa kinasubiri tu siku ambayo baba yake atazaliwa kisha naye azaliwe.

Hata hivyo, amini usiamini, inasemekana kuwa jamaa huyu alimwambia mpenzi wake Tanasha asijifungue kwanza angoje siku ya kuzaliwa kwake kisha ajifungue mtoto yule.

Aisee, kama huu uhondo ni wa kweli basi Daimond ni staa kivyake tu!

Jamaa ya karibu ya Diamond, mama yake, baba yake wa kambo na mpenzi wake walikuwa kwenye chumba cha hospitalini kusherehekea kuzaliwa kwa mjukuu wao wa nne na siku ya kuzaliwa kwa Diamond.

Kwa vile chanda chema huvishwa pete, kutoka kwa Radio Jambo, tungependa kumpongeza Kidosho Tanasha kwa kujifungua kitoto kizuri na kumtakia Diamond heri njema ya siku yake ya kuzaliwa.