Mwanahabari aliyekejeli ushindi wa Kipchoge akemewa mtandaoni

"Binadamu hadhibitiki akiamua kutenda"

Hiyo ndiyo ilikuwa kaulimbiu ya bingwa wa riadha ya masafa marefu Eliud Kipchoge alipoandikisha historia ulimwenguni kwa kukimbia mbio hizo chini ya masaa mawili.

Eliud Kipchoge ambaye alikata utepe baada ya saa 1.59.40 aliweka historia katika ulingo wa riadha kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza  mbio za masafa marefu kukatika kuda huo.

Hata hivyo, shirika la riadha ulimwenguni IAAF ilikosa kuhalalisha na kuthibitisha rekodi hiyo mpya ikisema kwamba Kipchoge hakukimbia katika mandhari ya kawaida. IAAF ilisema kwamba hakukuwa na mshindani mwingine katika riadha hiyo pamoja na kukosa kutimiza sheria zingine za IAAF.

Kipchoge  ambaye alipongezwa kote ulimwengumi akiwemo  rias wa zamani wa Marekani Barack Obama kwa juhudi zake na kuonesha ulimwengu kwamba hakuna kisichowezekana katika maisha ya binadamu.

Lakini kwa mwanahabari Paul Bisceglio,  mafanikio ya Kipchoge katika ulingo wa spoti hayakuwa na manufaa yoyote. Katika kauli yake kwenye mtandao, Biscegilo alikejeli ushindi wa Kipchoge akisema kwamba ushindi ulikuwa bandia.

https://twitter.com/PaulBisceglio/status/1183420536698916864?s=20

Maneno hayo yaiibua gumzo huku akikemewa na mashabiki wake Kipchoge ambao wanamtazama kama kielelezo bora katika maisha yao.

Architect Kyaka@jackaloh
The author should be reminded that the current World Marathon Record is held by the same person. He was not running to break his own record but to inspire and show others it can be done in under two hours.
"Mwandishi anafaa kukumbushwa kwamba yeye ndiye mmliliki wa rekodi ya dunia katika mbio hizo. Hakuwa anakimbia kuvunja rekodi tena, bali alitaka kuthibitishia dunia kuwa inawezekana chini masaa mawili.
 Gathoni @I_am_Gathoni
"Where were these thoughts BEFORE the race? Bile because a black man did it"
Alimwuliza kwamba mbona hangetoa maoni haya kabla ya riadha hiyo ? Au ana kinyongo kwa sababu ni mwafrika alishinda.
Japheth Odonya @odonya   Kamati ya roho chafu

https://twitter.com/AfroMelanated/status/1183488694126370817?s=20

@AfroMelanated alimkejeli kwa swali kwamba iwapo anasingizia kwamba maziwa mala ilimpa nguvu zaidi.