Martial anatarajiwa kucheza dhidi ya Liverpool baada ya kuregelea mazoezi

Anthony Martial anatarajiwa kuregelea mazoezi ya timu ya kwanza wiki hii na ana fursa ya kucheza katika mechi ya Manchester United dhidi ya mahasimu Liverpool jumapili. Mshambulizi huyo amekua nje tangu Agosti na jeraha la paja na United wamepata shida ya kufunga mabao alipokua hayuko. Lakini huenda akapiga jeki kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer watakapochuana na viongozi hao wa ligi ya Premier.  Hatma ya Paul Pogba, Aaron Wan-Bissaka, Victor Lindelof na Luke Shaw bado haijulikani ingawaje Jesse Lingard na Mason Greenwood huenda wakacheza.

Meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri angependelea mchezaji wa zamani wa safu ya ulinzi ya Manchester United Patrice Evra, ambaye alimfunza huko Turin kujiunga na makocha wasaidizi Old Trafford ikiwa atateuliwa kuwa meneja wa timu hiyo. Kwingineko Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anamtaka mlinzi wa zamani wa Chelsea Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, na kiungo wa kati Mfaransa N'Golo Kante mwenye umri wa miaka 28, kuondoka Stamford Bridge kuelekea Juventus.

Mechi ya Uingereza ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 huko Bulgari ilisimamishwa mara mbili kuwaonya mashabiki dhidi ya tabia za ubaguzi wa rangi. Mara ya kwanza mechi hio ilisimamishwa kunako dakika ya 28 huku Uingereza ikiongoza 2-0 na ya pili katika dakika ya 43 na kuanza tena baada ya majadiliano na meneja wa Uingereza Gareth Southgate. Uingereza ilishinda mechi hiyo 6-0 na kusalia kileleni mwa kundi A.

Mabingwa wa dunia Ufaransa walitoka sare ya 1-1 na Uturuki jijiji Paris na kuchelewesha kufuzu kwao kwa michuano ya Uro mwaka 2020.  Mshambulizi wa Chelsea Olivier Giroud alifunga bao dakika nne baada ya kuingia kama akiba kunako kipindi cha pili, huku Kaan Ayhan akisawazishia Uturuki dakika tano baadae.

Matokeo haya yana maana kuwa Uturuki inasalia juu ya Ufaransa katika kundi H.