PATANISHO: 'I am busy muache kunilazimisha kuzungumza!' - Paul

Catherine, 28,aliomba apatanishwe na mumewe bwana Paul, 30, ambaye wameishi pamoja kwa miaka sita.

Wawili hao wana mtoto mmoja ambaye amesaia na Catherine. Anasema kuwa mumewe hamshughulikii mwanao.

Kulingana na Catherine,

"Alikuwa mgonjwa na akaamua aende akatibiwe nyumbani kwao, na sasa akiwa kule alinyamaza na hakuwa anawasiliana nami. Ilifika mahali nikamaliza shule lakini sikuwa na karo ya kwenda college na kuna mtu ambaye alikuwa anilipie kisha anikate polepole.

Bwanangu aliposkia niko college alianza kusema kuwa nimepata mume mwingine na tangia Mei hajawahi rudi. Isitoshe alipopata nafuu aliniomba nimtumanie nauli lakini kila mara nikituma hajawahi kuja."

"Noo I'm busy my friend hata kama unapiga kutoka Radio Jambo. Why would you want to force me?" Alisema bwana Paul pindi tu alipopigiwa simu kabla ya kuskika akinung'unika na marafiki zake.

Hata hivyo Catherine aliongeza akisema,

Kuna msichana ambaye amekuwa akimchukua na kwenda naye kulala naye lodging na isitoshe alikuwa ananiambia kuwa mie ni mke ambaye sijasoma. Nimekuja nimepata kazi ya kufunza hapa na ninapata fedha, nang'ang'ana nipate fedha ili nilipe karo.

Juhudi zetu za kumfikia Paul kwa mara nyingine tena hazikufua dafu na hapo ikabidi tuwaachie wanajambo waweze kumpa Cate mawaidha.