Mwanaume apigwa na kuuawa baada ya kushindwa kulipa deni la sh100

Mwanume mmoja mwenye umri wa miaka 25 kutoka kijiji cha kajoro kaunti ndogo ya Teso kusini kaunti ya busia amepigwa na kuuawa katika kituo kimoja cha pombe haramu ya chang’aa katika soko la tangakona kaunti ndogo ya nambale kaunti ya busia baada ya kushindwa kulipa deni la pombe la shilingi mia moja.

Wanafamilia wa Dennis Juma Oita wanasema kuwa marehemu alipigwa na tofali shingoni na kujeruhiwa vibaya huku akiaga dunia alipokuwa anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya busia.

Wanafamilia hii wamewalaumu maafisa wa polisi kwa kushindwa kuwakabili wauzaji wa pombe haramu katika soko la tangakona.

Hayo yakijiri, Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja ametoa onyo kali kwa maafisa walaghai katika sekta ya afya wanaohusishwa na wizi wa madawa hospitalini kuwa watakabiliwa kisheria.

Anasema baadhi ya maafisa katika sekta hiyo wamekuwa wakiiba dawa katika hospitali tofauti katika kaunti hiyona hivyo kusababishia kaunti hiyo hasara.

-Leonard Acharry na Solomon Muingi