(+ Video ) Mpiga picha Collins Kweyu afunguka baada ya kichapo na Mike Sonko

Mpiga picha wa Standard Media Group Collins Kweyu amefunguka baada ya kupokea kofi la kinyama kutoka kwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko hapo jana.

Sonko alikuwa ameandamana na wafuasi wake katika ofisi za EACC.

EACC ilikuwa imemuita gavana huyu kujibu maswali yanayoendeshwa ili kubaini iwapo kuna ubadhirifu wa hela au la.

Kwa hasira za mkizi, Sonko alimwangushia kofi hatari mpiga picha Collins.

https://www.instagram.com/p/B4g4nYZlzCn/

Baadaye umati ulianza ulimpiga mpiga picha huyu. Katika video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, jamaa mwenye koti ya buluu anaonekana akimpiga Kweyu.

"Nilijipata napigwa na watu na singebaini aliyekuwa ananipiga bila kosa lolote..." Kweyu alisimulia NTV

Wengi wamekashifu kitendo hicho cha kinyama huku baraza la vyombo vya habari nchini MCK (Media Council of Kenya) ikichapisha waraka kulaani utovu huo wa maadili.

MCK imeomba ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya jinai (DCI) na mkurugenzi wa mashtaka ya umma (MCK imeomba ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya jinai (DCI) na mkurugenzi wa mashtaka ya umma (