Je, wajua Papa Francis wakati moja alikuwa Bouncer kilabuni?

Papa Francis alichaguliwa mnamo Machi 2013 katika kanisa la kikatoliki baada ya Papa Benedict XVI kustaafu.

Yeye ni Papa wa 266 nchini Roma kushikilia uongozi katika kanisa hilo.

Ila kile watu wengi hawajui ni kwamba jina rasmi la Papa Francis ni Jorge Mario Bergoglio.

Aidha, kabla ya kujiunga na kanisa hilo la Kikatoliki alipitia maisha magumu sana. Alilelewa katika mazingira  yenye changamoto tele. Wazazi wake walihama na kutoroka dhuluma za kiongozi Benito Mussolini.

Na ili kujikimu, ilimbidi Papa Francis kufanya kazi kuwa bawabu wa usiku katika baa moja kwa takribani mwaka nchini Buenos Aires..

Na wakati wa mchana alifanya kazi za usafi katika baa hiyo. Ni vigumu kuamini, ila mja hupata ajaliwalicho silo atakalo.