Kijana ashtakiwa na kufanya mtihani wa KCSE kortini

Amini usiamini, mwanafunzi mmoja kutoka mji wa Narok anafanya mtihani wake wa KCSE kortini baada ya kushtakiwa na kufungwa kwa madai ya ubakaji.

Dogo hili jina lake Gideon Chepkwony mwenye umri wa miaka 19, mwanafunzi wa shule ya upili ya Royal Vision alitiwa mbaroni jumanne na hakimu Wilbroda Juma baada ya kushtakiwa kumbaka binti mmoja tarehe 14 mwezi wa kumi mji wa Narok.

Mbali na hayo,kijana huyu alishtkiwa pia kwa kosa la kuwa na binti mdogo kwa njia isiyo furahisha mbele ya mahakama.

Juma alituma ujumbe kwenye afisi ya mtihani na kuomba usalama wa kulinda mtihani wa mshukiwa huyu. Zaidi ya hayo, Juma aliliamuru afisi yake ya Narok kuhakikisha kuwa usalama wa mtoto huyu pamoja na mtihani wake umesisitizwa.

Jamaa huyu Chepkwony alisimama mbele ya mahakama miezi kadhaa iliyopita na kushtakiwa kwa kosa lile lile lakini akakataa mashtaka hayo na kuachiliwa baada ya kulipa shilingi 200,000.

Wakati huu jamaaa huyu hakuachiliwa kwa sababu mama yake alipatikana akijaribu kuhonga mshtaki ili aweze kukomesha kesi hii na ndipo Juma akaamua kumweka Chepkwony rumande.

Kesi hii itaskizwa tarehe 21 Novemba.