Lebo ya WCB kutumia uganga kuzuia mvua Dar Es Salaam, Babu Tale

Babu-Tale-and-Diamond
Babu-Tale-and-Diamond

Boss Tale amefungukia Bongo 5 kuwa wanafanya wawezalo ili kuzuia mvua isinyeshe.

WCB ina fiesta kubwa sana Dar Es Salaam ambayo itakuja mastaa kama Wizkid, Tiwa Savage kati ya wengineo.

'Nikwambie hapa tulipo tunahangaika sana kupigia waganga simu."

"Unawaza nani anakuzuilia mvua so tunatoka nje ya box..."

"Its normal we are African, ata wewe unafanya usininyoshee kidole..." Alisema Boss Tale.

Tale alikuwa anazungumzia harakati wanazofanya ili kuhakikisha fiesta ya Wasafi katika uwanja wa posta imekuwa shwari.

Aidha, Tale amefunguka jinsi muziki unavyolipa hela kibao huku akimtaja Diamond Platnumz kama mtu anayependa kuwekeza.

"Diamond anaweza kuwekeza hela kwa msanii bila kuogopa lolote ..."

Tale ni mojawapo wa mameneja wa lebo ya WCB akiwemo Sallam SK na Mkubwa Fella.

Tale amesema kuwa anamwangalia Fella kama ndugu yake.

Ametaja mchango mkubwa zaidi wa Fella katika muziki wa Bongo Fleva.

Haya yanajiri huku Mondi akiangusha ngoma kubwa ya Baba Lao itakayokonga nafsi mashabiki wao fiesta la Kijitonyama.

Ngoma hii ilileta utata na kufanana na Soapy ya Naira ila S2Kizzy akaweka wazi.

Producer huyu wa mkwaju wa ‘Baba Lao’ ya Mondi ametokezea na kufunguka kuhusu midundo ya ‘Baba Lao’ na ‘Soapy’ ya Naira kufanana.

Akihojiwa na kituo cha Wasafi FM nchini Tanzania, S2Kizzy amesema kuwa waliomba ruksa ya kuimba na mdundo huo.

Producer huyu ameeleza kuwa alivutiwa zaidi na mdundo wa Naira katika ngoma ya Soapy.