Mariga akubali kubwagwa, amualika Imran chakula cha mchana - Video

Mgombeaji wa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra McDonlad Mariga amekubali matokeo ya uchaguzi.

Mariga akimpongeza mshindi wa uchaguzi huo Imran Okoth wa ODM alisema kufurahishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Kulingana na kanda ya video, Mariga anaonekana akisema, "Ni Mariga, nimepiga nikuambie congratulations. Kura imekua poa hatujapigana, meeting tulikuwa pamoja na pia niko ready for lunch."

https://twitter.com/TheStarKenya/status/1192534180061679618?s=20

Alisema kwamba yuko tayari kumuunga mkono Imran kuhakisha kwamba wakaazi wa Kibra wanahudmiwa ipasavyo.

Baada ya uchaguzi, tuendeleze maisha yetu ya kawaida na kudumisha urafiki wetu," Mariga alisema.

Akijibu salamu hizo za pongezi na pongezi, Imran kupitia ukurasa wake wa Twitter alimlibikizia sifa Mariga kwa kukubali matokeo na hata kumuunga mkono katika utendaji kazi wake.

Katika uchaguzi huo, Imran Okoth wa ODM ndiye  mshindi kwa kura  24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Eliud Owalo wa ANC alipata kura elfu 5,275.