Unajua yepi kumhusu mbunge mteule Imran Okoth? Soma hapa

EIR-rD8WoAET4qF
EIR-rD8WoAET4qF
Imran Okoth sasa ndio jina na ambalo linatajwa sana kwa ushindi mkubwa eneo bunge la Kibra.

Ni mwanasiasa shupavu na ambaye alipanga vizuri siasa kutoka siku ya kwanza hadi kufikia awamu ya kutangazwa mshindi.

Ila je? Unajua yepi kumhusu Imran?

Jina la Imran limejulikana kwa sana baada ya kifo cha nduguye Ken Okoth.

Aidha, ata kabla kifo kumkuta Ken, jina la mwanasiasa huyu lilianza kutajwa katika vyombo vya habari.

Kando na kuwa ni kakake Ken Okoth, kuna baadhi ya vitu unafaa kufahamu kuhusu Imran.

Imran ni mzawa wa Kibera, mtaa wa Kisumu Ndogo.

Amezaliwa pamoja na ndugu watano akiwemo marehemu Ken Okoth.

Alikuwa msaidizi wake Ken Okoth

Kipindi na ambacho kakake Ken Okoth alikuwa mgonjwa, Imran alihakikisha miradi iliyoanzishwa Kibra inaendelea.

Imran pia alikuwa mwenyekiti wa baraza la eneo bunge lililotwika jukumu la maendeleo (CDF) kwa miaka 7.

Kazi hii imempa hekima ya kuendesha Kibra kama mbunge.

Imran ni mnyamavu. Hii ina maana kuwa kiongozi huyu si wa maneno mengi.

Hotuba anazochapisha katika mitandao ya kijamii, kampeni zake ni ishara kuwa Imran sio mtu wa kuongea sana.

Hii inamuweka tofauti sana na wanasiasa wanaopenda kuongea kwingi bila maendeleo yoyote.

Imran ana mke na hapendi sana kuifanya ijulikane. Mahusiano yake na mpenzi wake ni siri kuu sana.