Jamaa ambaye aliyepita na shemeji yake alalamika kuchezwa pia 

massawe.
massawe.
Kuna msemo husema dunia duara. Msemo huu huashiria shepu ya dunia lakini maana yake ni kuwa hata uende wapi bado utarudi nyumbani.

Hata hivyo katika muktadha huu, natumia msemo huu kuashiria kuwa chochote umfanyiacho mwenzako siku moja kitarejea kwako kama adhabu.

Msemo huu autambuaye vyema ni jamaa kwa jina Sylvester, ambaye sasa amebakia na uchungu na machozi tele akilipia makosa au dhambi alizotekeleza siku za nyuma.

Akizungumza na Massawe Japanni kwenye kipindi cha Bustani la Massawe, jamaa huyu alifichua kuwa walitengana na mkewe baada ya kupatikana akimnyemelea dadake (shemeji yake).

Alidai kuwa mkewe alimtenga naye akaamua kumuoa dadake na huku akidhani ameangukia dili nono hakujua kilichomngoja siku za usoni.

Sylvester ambaye ni dereva wa masafa marefu alipewa fununu kuwa mkewe huleta wanaume kwake kila anapoondoka. Siku moja alifunga safari na kurudi nyumbani na amini usiamini alimfumania mkewe na jamaa mwingine kwake.

Skiza usimulizi wake,

Nilioa dada ya mke wangu haki najuta sana, mke wangu alimleta kwa boma na tulikuwa tunaishi pamoja na ile tamaa ya mwanaume ikaniskuma.

Mke wangu alipojua aliniacha na nikamuoa dadake, sasa siku hizi nikiwa kazi zangu niliskia fununu kuwa kuna jamaa huja kwangu. Siku moja baada ya kurudi nilipata mwanaume kwa nyumba.

&feature=youtu.be