Atwoli amshauri Ruto kumwomba msamaha Mzee Moi ili kumrithi Uhuru

Katibu mkuu wa Cotu Francis Atwoli amesema kwamba itakuwa vigumu sana kwa Naibu wa Rais William Ruto kumrithi Rais Uhuru Kenyatta hadi atakapozingatia maadili ya unyenyekevu.

Atwoli ambaye alizuru ngome ya Ruto mjini Eldoret alisema kwamba Ruto anakumbwa na vizingiti vingi na alimshauri kumwomba msamaha Rais mstaafu Daniel Moi.

Alimshauri Ruto kupitia Seneta wa Baringo Gideon Moi akutane na Mzee Moi ili apewe baraka za mzee anapotazamia madaraka ya juu.

"Iwapo hatafanya hivyo basi itakuwa vigumu kwake kuchukua uongozi 2022," Atwoli alisema.

Alizungumza hayo katika halfa ya kuchangisha pesa katika kanisa la Evangelical Bible mjini Eldoret ambapo aliambatana na wabunge Joshua Kutuny wa Cherangany, Sila Tiren wa Moiben na Wilson Sossion ambaye ni mbunge mteule.

"Ninamshauri Ruto hasipuuze wito huu iwapo anataka kiti cha urais," alisema.

Miezi mitatu iliyopita, katibu  huyo wa Cotu alizua tafaruku aliposisitiza kwamba jina la Ruto halitakuwa miongoni mwa watakaogombea kiti cha urais 2022.

Akita Eldoret, Atwoli alisema kwamba iwapo Ruto hatapatana na Moi, hasahau azma ya kurithi rais Uhuru.

Hata hivyo juhudi za naibu wa rais William Ruto za kufika Kabarak nyumbani kwake Moi kumeambulia patupu.

Baada ya kusemekana kuwa Seneta wa Baringo Gideon Moi kumzuia Ruto kukutana na mzee.