PATANISHO: Kijana wa ukoo wangu alimpachika mwanangu mimba

Leo katika kitengo cha patanisho na Gidi na Ghost asubuhi aliyeomba kupatanishwa ni jamaa kwa jina Billy aliyetuma ujumbe mrefu akidai,
Nilikuwa na msichana fulani ambaye nilimpa mimba na mama mkwe alitutenganisha hadi akashawishi mwanadada atoe mimba. Nilikasirika na nikanywa sumu lakini kwa bahati sikuaga dunia. Sasa nataka kuomba msamaha kwa mama mkwe kwa kitendo nilichofanya kwao.

Alipopigiwa simu alizidi kusema,

Sasa tulikuwa tumeishi na huyu msichana kwa miezi mitatu na niligundua kuwa huyu msichana alikuwa amenidanganya. Aliniambia amemaliza kidato cha nne na kumbe alikuwa ameambiwa arudie shuleni lakini akapotea.

Billy anadai kuwa alikuwa amempachika msichana mimba na mama mkwe aliposkia vile alimtoa nyumbani baada ya kumnyang'anya fedha na kila kitu chake.

Isitoshe sahii Billy ameoa mwanamke mwingine tayari na wawili hao wanatarajia mtoto.

Sina mda kwani pia yeye mwenyewe anajua chenye alifanya na umwambie mimi bado ni kahaba na sijawacha bado. Mama Eunice alisema pindi tu alipopigiwa simu.

Baada ya hilo, bwana Billy anasema kuwa lengo lake ni kumuomba aliyekuwa mama mkwe msamaha kwani yule mwanadada alimweleza kuwa mamake anadai kuombwa msamaha. Hata hivyo mama alisema kuwa hayo ni maneno yake kwani msichana tayari alirudi nyumbani.

Huyo alisema kuwa atarudi tena kwangu kujitia kitanzi na nangoja sana." Mama Eunice alisema akiongeza kuwa hawezi msamehe Billy na hawezi msamehe.

Cha kushangaza ni kuwa Billy na mama Eunice ni wa ukoo mmoja na kinachouma ni kuwa alimuendea mtoto wake kisha akajaribu kujitia kitanzi kwa boma lake.