Fayma azungumzia mimba ya Nana, asema sio ya Rayvanny

Rayvanny
Rayvanny
Mke wa staa wa muziki Rayvanny amesema kuwa Nana ana mimba ya miezi minne.

Akihojiwa na Global TV publishers, Fayma amesema kuwa wanaomhusisha Rayvanny na mimba ya Nana hawana akili.

"Mimi siwezi nikazungumzia chochote na huyo mdada kwa sababu amefanya tu wimbo na baba mtoto wangu lakini vitu zingine sizijui..."

Fayma amesema kuwa bwanake Nana alikuwepo kipindi Rayvanny anashoot video ya I Love You.

"Ninachokijua ni kuwa ni mjamzito wa miezi minne niliambiwa hivo na mwanamume wake the day of the video alikuwepo akimsimamia akifanya video..."

Matamshi yake Fayma yanajiri huku Rayvanny akikana taarifa za kutoka kimapenzi na Nana,

“Sipo kwenye mahusiano na Nana, tena ana mahusiano yake ambayo nayaheshimu sana sana.Kichupa ni kizuri kwani kinaonyesha ukweli na mapenzi yapo. Nilitaka video hiyo iwe jinsi ilivyo..” Rayvanny aliongeza.