PATANISHO: Mume wangu aliniambia nitaendea kifo krisimasi

Maureen, 24, kutoka Nyamira aliomba apatanishwe na mumewe bwana Denno Onduko mwenye umri wa miaka 27.

Alipopigiwa simu bi Maureen alisema,

"Mzee alikuja usiku ambao tulikosana akiwa amebeba samaki na akala vyema na watoto. Kulikuwa na mazishi hapo karibu na aliporudi alikuwa mlevi kupindukia na nikamuarifu hapaswi kuoga hadi asubuhi."

Aliongeza,

Baada ya kumwambia asijitandaze sakafuni akaamka na kunipiga mangumi huku nikiwa nimebeba mtoto"

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

Baada ya kukosa kumpata mumewe kupitia simu bi Maureen alifunguka zaidi kuhusu uhusiano wao.

Shida nimoja hapo awali alinitishia kuwa tukikosana naye atanipiga aniue kisha aniweka kwa kamba ni kama nimejinyonga. Aliniambia, hiyo sikukuu ya Krisimasi ukija jua unakujia kifo kwangu, hapo nikaogopa nikasema nikienda pekee yangu naendea tu kifo

Ujumbe, mimi nampenda bado na naomba anipigie simu tu aniombee msamaha kisha aje nyumbani kwetu ili tumalize hayo mambo yote.