(+ Picha) Diamond Platnumz abuni njia mpya ya kuwaongea na watoto wake

diamond-kids2-696x431
diamond-kids2-696x431
Staa wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz yupo mbioni kuhakikisha kuwa ametengeneza mazingira mazuri kati yake na watoto aliowazaa na Zari The BossLady.

Diamond hajakuwa karibu na wanawe Princess Tiffah na Prince Nillan kwa kipindi kirefu baada ya kutemana na aliyekuwa mpenzi wake Zari.

Mazingira ambayo sio mazuri yanaonekana waziwazi kwani Zari hakuweza kumualika katika sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwa Nillan.

Kupitia ujumbe wa Insta, Diamond alichukua nafasi hiyo kumtakia mwanawe heri katika siku hiyo muhimu.

Diamond Platnumz aliposti picha za Nillan na kuandika ujumbe kuwa anampenda zaidi.

Wawili hawa walitemana baada ya tuhuma za usaliti katika ndoa.

Kuna kipindi na ambapo Diamond aliwahi kunung'unika kuwa hapewi nafasi nzuri ya kukaa na watoto.

Diamond amewahi kukiri katika ngoma na kusema kuwa huwa anawaona watoto wake katika mtandao wa Insta.

Ili kuhakikisha kuwa ameziba pengo la baba kwa watoto, staa huyu aliamua kuwapigia simu katika mfumo wa video.

Tazama picha hapa: