Babake Diamond Platnumz amsifia aliyerithi mkewe Sanura Sandra

Screenshot_from_2019_12_17_11_30_02__1576571430_90740
Screenshot_from_2019_12_17_11_30_02__1576571430_90740
Babake Diamond Platnumz ametoa sifa nyingi na kumlimbikizia Shamte mpenzi wa sasa wa Sanura Sandra sifa kibao.

Ikumbukwe kuwa Sanura alikuwa mpenzi wake baba Diamond na wakatengana miaka ya awali.

Shamte alichukua usukani baada ya baba Mondi.

Babake Diamond amesema kuwa hana wivu naye katika mahusiano haya mapya.

“Ninampongeza sana Shamte kwa sababu anaisimamia familia vizuri, sina kinyongo naye kwa sababu kila mtu ana maisha yake, " Baba Diamond aliisimulia gazeti la Ijumaa Wikienda.

“Acheni wale maisha maana ni wakati wao! Maadam napata haki yangu kama baba, sioni ubaya kumsifia,” alisema baba Dangote.

Picha za wawili hawa ( Shamte na mama Diamond ziliteka hisia za wengi katika mitandao ya kijamii wikendi iliyopita.

Katika mahojiano ya hapo awali, Shamte alisimulia jinsi alikutana na mama Diamond.

"Tulikutana Paris, muulize yeye ndo anajua ila mtu akataka kuzungumza azungumze..."

Shamte alisema kuwa hachukii wakati na ambapo media zinawaandika kuhusu uhusiano wao

"Kwanza tunacheka, kwani wakati huwa tunapenda, tunajua na watu watuongelea vipi tusije tukajiona tuko sawa kumbe hatuko sawa..."