PATANISHO: 'Mimi sikutaki hata sikupendi!' Trizah amfokea Chris

Bwana Chris Nyongesa, 31, aliomba apatanishwe na mkewe Trizah, 266, akidai walisumbuana na akamtoroka
"Gidi nilipatikana nikizungumza na simu na mpango wa kando kumbe mke wangu alikuwa anaskiza yote hapo mlangoni. Alinigombanisha na hapo nikamzaba kofi na nikaondoka." Alisema.

Aliongeza,

Miaka tisa tumesumbuana na tumeishi maisha ya kijeshi na nataka mwaka wa 2022 tuishi kwa amani na yote yalisababishwa na mambo ya pombe. Mambo ya mipango ya kando niliwacha kitambo na nataka turudiane tuanze mwaka vyema.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka tisa na wawili hao wamejaliwa na watoto wanne.

Mimi mambo yako ya wanawake sitaki, nataka mtu mwenye mwelekeo, mtu mwenye ana deal na mtu mmoja." Alisema Trizah kabla ya kuongeza, Mimi sikupendi hata sikutaki!

Licha ya kuzomewa, bwana Chris bado anashikilia imani kuwa Trizah anampenda na kuwa hakuzimiwa simu ila simu yake ina shida.