Shabiki amjia juu Diamond Platnumz kwa kutomualika Wema Sepetu kwenye Tamasha

diamond-wema
diamond-wema
Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz amepata kero la mashabiki baada ya kukosa kumualika nyota wa filamu Wema Sepetu katika tamasha lake mwishoni wa mwaka huu.

Baadhi ya wafuasi wanaamini kuwa mrembo huyu ana mchango mkubwa katika ufanisi wa staa huyu.

https://www.instagram.com/p/B6lPra8pRy8/

“Kwa jinsi alivyomsaidia mpaka akafika hapo alipo, Diamond alitakiwa kumwalika na kumposti Wema kama alivyofanya kwa hao wengine hata kama wamekosana kiasi gani, ni kosa gani hilo kubwa asisamehe na kuendelea na maisha kama kawaida,” mfuasi wa Diamond aliandika Insta.

Diamond amekuwa akiwaalika mastaa wengi Tanzania katika tamasha lake.

Katika posti la Insta la kuwakaribisha wasanii wakubwa Tanzania katika tamasha la kufunga mwaka mjini Kigoma, Mondi amemkaribisha Mwarabu na kuchora ujumbe huu.

" Amini kwamba Diamond Platnumz alijengwa na anajengwa na watu wengi ambao usiku na mchana wanapambana kuhakikisha kwa pamoja na kijana wao tunafikisha sanaa yetu Mbali... My brother  KIGOMA inakusubiri ikupe Shukran za Dhati...."

Posti ya staa huyu inaonyesha kuwa hakuna bifu iliyopo kati yake na Mwarabu Fighter ata kama alimpiga kalamu.

Ila je? Unafikiri kuwa ni freshi kutomposti Wema Sepetu. Toa mchango wako