(+Video ) Alivyopokelewa Diamond Platnumz Kigoma, miaka 10 kwenye sanaa

2017-09-06-08.36.28-1
2017-09-06-08.36.28-1
Umati mkubwa wa mashabiki ulijaza ukumbi kwa Kigoma kumpokea staa wa muziki Diamond Platnumz.

Msanii wa kizazi kipya na mkurugenzi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz alifanya bonge la tamasha mjini Kigoma ili kuadhimisha miaka 10 ya uchapakazi katika tasnia ya muziki.

Tazama jinsi alivyopokelewa Kigoma:

https://www.instagram.com/p/B6qtZpAJ5bQ/

Sherehe hii ilifanyika kwao Kigoma na aliweza kuwaalika mastaa wengi ili kuwapa burudani tele.

Safari ya muziki ya nyota huyu wa bongo fleva ilianza mwaka wa 2009 na kufikia sasa amepiga hatua kubwa pamoja na kuupeleka muziki wa afrika mashariki katika upeo wa juu zaidi.

Diamond ameweza kutoa mchango mkubwa katika jamii huku akiwatoa kimuziki mastaa kama Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Mbosso pamoja na Lavalava.

Kando na mchango huo wa kupigiwa mfano , Diamond ametengeneza ajira kwa wanahabari kwa kuanzisha kituo cha redio na runinga Wasafi FM na Wasafi TV mtawalia.