Sifa 5 za wanawake wa jamii ya Waluhyia, uchapakazi unaongoza

lUHYA-696x418
lUHYA-696x418
Katika kila jamii, zinakuwepo sifa watu wa eneo hilo uhusishwa nazo.

Katika orodha hiyo ya vigezo, wanawake wa jamii ya waluhyia wanaonekana na sifa nzuri za kuwasetiri wanaume wao.

Sifa za wanawake katika jamii hii zinaanzia jinsi wanavyopika, uchapakazi na uaminifu katika ndoa.

Tumesogezea hapa baadhi ya vigezo vya wanawake hawa

Moja, wanawake waluhyia wapishi kweli,

Wanawake kutoka jamii wanapigiwa upatu wa kuwa hodari jikoni.

Yaani ukimuoa mwanamke kutoka jamii hii chakula na lishe yako zitakuwa imara sana.

Pili, wanazingatia usafi mno,

Wanawake wa kutoka eneo hili wanatajwa kuwa watu wanaopenda usafi sana.

Usafi unatajwa kuanzia katika vyumba vyao huku wengi wakipata ajira kama vijakazi na mama wa kufua katika miji mikuu.

Tatu, Ni wachapakazi sana

Taifa ya Mulembe inapigiwa mfano mzuri kwa kuwa na warembo wanaopenda kazi.

Mwanamke wa jamii hii atatamani kusalia mashambani na kuchapa kazi katika shamba.

Nne, ni waaminifu sana

Inaaminika kuwa ni nadra sana mwanamke kutoka jamii hii kuchepuka.

Inaaminika kuwa wanajenga misingi dhabiti ya familia na kujenga ndoa nzuri.

Tano, Ni warembo sana

Kutoka utosini hadi kwa miguu, waluhyia wanaaminika kuwa na umbo nzuri.