Bonge la smile, Ghost Mulee aposti picha na kijana wake

Screenshot_from_2020_01_06_10_28_30__1578295741_55475
Screenshot_from_2020_01_06_10_28_30__1578295741_55475
Mtangazaji wa kituo hiki Ghost Mulee amemtambulisha kijana wake katika mtandao wa kijamii wa Insta.

Ni nadra sana kumwona staa huyu wa utangazaji na mwanasoka akifanya kitu kama hiki.

" Baba na mwanawe wanawatakia siku njema ya Jumapili," alichapisha Ghost.

https://www.instagram.com/p/B675iHBlTPa/

Ghost alikuwa kocha wa zamani wa timu ya kitaifa ya Harambee Stars na kujiuzulu kwa kile alikitaja kama ' upuzi wa watu kutolipa mishahara'

Katika mahojiano ya awali na kituo hiki , Ghost alisema kuwa kuchelewesha kwa mishahara kulichangia sana kujiuzulu kwake.

"Maswala ya kulipwa yalikuwa ni tatizo kubwa. Nawadai milioni kadhaa. Nimekuwa na rais wa shirikisho akanieleza kuwa wanakifa wataleta hela yangu kwa matanga haraka sana..."

Hata hivyo, Ghost bado yupo katika maswala ya soka kupitia Liberty Academy ambayo anaitumia kukuza talanta nchini.

Ghost alisema kuwa sasa anachokipanga ni kuinua talanta za vijana wengi nchini.

"Sasa hivi tunaipanua academy. Angalia siku zijazo tutakuwa na academy kubwa sana tutakayokwenda kuanzisha hapa jijini Nairobi."

Huku akionyesha tabasamu, Ghost alisema kuwa yeye na soka hawawezi kutengana.

"Damu yangu ni kabumbu kwa hivyo siwezi nikaacha maswala ya kabumbu."