'Diamond anahofia ndoa,' Asema dadake, Esma

Esma Khan, dadake Diamond Platnumz amesema kwamba mwanamziki huyo anahofia sana kufunga ndoa kabla ya kujiandaa.

"Sisi hujadiliana sana kuhusu masuala ya ndoa, [Diamond] ni mtu anayehofia sana kujiingiza kwenye ndoa. Anataka ajiandae ipasavyo kabla ya kuamua kufunga pingu za maisha" 

Itakumbukwa kuwa, Diamond alisogeza mbele ndoa yake na Tanasha iliyokuwa imepangiwa siku ya wapendanao 14, 02, 2019. Tanasha alisema harusi ilikosa kufungwa kwa kuwa familia yake hawakuwepo.

Hizi majuzi, aliambia Wasafi Media kwamba mwaka huu wa 2020 ataweza kumuoa Tanasha

"Tumuombe Mwenyezi Mungu atubariki Inshallah mwaka unaoingia itakua zamu yangu maanake ndugu zangu wte washaaondoka."

"Sina sababu yangu mimi kuchelewa kuoa wakati nin akila sababu ya kuweza kuoa. Nina mwanamke mzuri, amenizalia mtoto mzuri, riziki ya kula sikosi, nina marafiki wazuri."

Kabla hajapatana na Tanasha, Diamond alikua amepanga harusi na aliyekua mpenzi wake Zari Hassan na kusema kuwa, harusi hiyo itakua ya kimataifa. Aidha, Zari alimwandikia arafa ya utengano kwenye mtandao wa Instagram mnamo 14,02,2018.

Inasemekana kuwa, Diamond kutaka kumuoa Tanasha siku kama hiyo (Siku Ya Wapendao) ni kama kulipa kisasi kwa Zari.