Kasisi amchoma mkewe kisu mbele ya kanisa, ajipasua koo

KANISANIII__1578303632_87148
KANISANIII__1578303632_87148

Wingu la simanzi liligumbika kanisa la Ground For Jesus lililopo mtaa mmoja eneo la Mombasa baada ya kasisi anayefahamika kama Elisha kumdunga kisu mkewe hadi kumuua.

Wawili hawa wanadaiwa kuwa na migogoro ya kifamilia iliyopelekea kisa hiki kufanyika.

Kasisi Elisha wa kanisa la Ground for Jesus alivamia mkewe mbele ya kanisa la kumdunga kisu kikali.

Mkewe alikata roho na kufariki papo kwa hapo huku Elisha akijipasua koo kwa kisu na kuangamia.

Waumini wamesema kuwa juhudi za kuwaokoa wawili hao hazikuweza kuzaa matunda kwa kasisi huyo alifanya unyama huo kwa kasi.

 Kamanda wa Polisi wa eneo la Kisauni, Julius Kiragu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Aidha, Kiragu amedokeza kuwa kuna nyaraka kumi na saba zilizopatikana katika mfuko wa jamaa huyo zitakazosaidia uchunguzi.