INSTANTLY! Paspoti na Vitambulisho kutolewa papo hapo-Matiang’i

Matiangi
Matiangi
  Kuanzia Julai tarehe moja mwaka huu  stakabadhi muhimu kama vile  Vitambulisho ,Paspoti ,na vyeti vya kuzaliwa/vifo  vitakuwa vikitolewa siku iyo uliotuma maombi ya kupewa . Tangazo hilo limetolewa  na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I akiwa huko Mombasa . Lakini ameongeza kwamba maombi yanayotoka nje ya Nairobi au nje ya nchi yatachukua  siku kadhaa kushughulikiwa

.Amesema  haifai kwa wakenya kuendelea kupitia mahaingaiko kabla ya kupata stakabdhi hizo .“ Tunatangamana na wananchi wetu kila siku hasa wakiwa wanyonge na mateso nilioona wakipitia mwaka jana sio jambo linalofaa kukubalika’ .Amesema  waziri huyo.

“  Hatuwezi  kuchukuliwa kama watoaji wa suluhisho ilhali wakati huo huo tunakuwa chanzo cha machungu . Hili lazima likome!’ amefoka Matiang’I . Waziri huyo amemwagiza katibu wa kudumu anayeshughkilia  huduma za wananchi kuhakikisha kwamba  ahadi za utendakazi na uadilifu wa idara za  serikali  zinatekelezwa . Pia amewaagiza makamishna wa kaunti kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika  vituo vya kutoa huduma za serikali  na kuripoti hatua zinazofaa kuchukuliwa kuboresha utendakazi na utoaji wa huduma kwa wnaanchi .