Baadhi ya wanafunzi walionusurika katika kisa cha mkanyagano katika shule ya msingi ya Kakamega kilichosababisha vifo vya wenzao 14 wamedai kwamba mwalimu mmoja alikuwa akiwafukuza waondoke shuleni baada ya masomo jioni . Hata hivyo haijatolewa taarifa rasmi ya kueleza sababu ya kisa hicho ambacho kimewatamausha wengi .
Wazazi waliowapoteza wanao wamefurika katika hospitali ya rufaa ya kakamega ili kuitambua miili ya watoto wao . Waziri wa elimu George Magoha ,katibu wa kudumu Belio Kipsang na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya walizuru shule hiyo siku ya jumanne asubuhi ili kutathmini hali . Wengine waliozuru shule hiyo ni seneta wa kakamega Cleophas Malala , seneta wa zamani wa kaunti hiyo Bony Khalwale na msemaji wa serikali Cyrus Oguna .