Kitaumana: Diamond aonekana na Hamisa baada ya kumuacha Tanasha Nairobi

hamisa
hamisa
Kwa kweli kulingana na matukio ya hivi karibuni, ni dhahiri kuwa kuna mambo yanayoendelea katika uhusiano wa Diamond Platnumz na Tanasha Donna.

Wiki iliyopita, Tanasha alizindua kanda yake ya kwanza kwa jina, Donnatella, hapa jijini Nairobi.

Kuharibu mambo, mpenziwe Diamond ambaye alikuwa nchini kuhudhuria hafla hiyo, alimuacha na kurudi Tanzania huku akiambatana na Mbosso.

Kulingana na mwandani wetu, Diamond hakufurahishwa na jinsi alivyopokelewa katika uwanja wa ndege.

“DIAMOND AND HIS WCB CREW WERE VERY DISAPPOINTED AFTER THEY ARRIVED AND FOUND NO MEDIA AT THE AIRPORT TO WELCOME THEM AND COVER THEIR ARRIVAL. THEY WERE SO ANGRY, AND IT SHOWED IN THE WAY THEY RESPONDED TO JOURNALISTS AT THE PRESS CONFERENCE.” mwandani wetu alisema.

Kulingana na tetesi katika mitandao ya kijamii, Diamond Platnumz alondoka na kwenda kuburudika na mpenzi wake wa zamani, Hamisa Mobetto.

Mbali na Hamisa kuonekana akiendesha gari la msanii huyo, Diamond alikuwa mle ndani. Kanda kadhaa zilichapishwa kabla ya kufutwa na wanabllogi wa Tanzania.

Wawili hao bado hawajazungumzia kuhusu kisa hicho.

Hata hivyo, dadake Diamond, Esma Dangote, alikuwa na mawili, matatu ya kusema kuhusu tukio hilo.

“PEOPLE KEEP SAYING THAT HAMISA AND DIAMOND ARE BACK TOGETHER BUT THAT IS NOT TRUE. THOSE ARE PURE LIES BEING PEDDLED.”alisema.

aliongeza,

I DON’T LIKE SUCH LIES BECAUSE WHEN PEOPLE START SPREADING SUCH RUMOURS IT IS HARMFUL. ALL THE SAME, PEOPLE WILL STILL TALK.

Baadaye Esma alimpa Tanasha maneno ya kumpa moyo akimshauri kutoskiza umbea.

I BEG YOU TANASHA TO CONTINUE YOUR RELATIONSHIP WITH YOUR LOVER [DIAMOND] DO IT WITH AS MUCH EASE AS YOU CAN MASTER. BE COMFORTABLE IN THE LOVE YOU TWO SHARE. REST IN THE REASSURANCE THAT THERE IS NOTHING GOING ON BETWEEN THE TWO.”

Hapa sasa kwa kweli kuna uhondo ambao unaiva na baada ya mda usiokuwa mrefu tutajua mbivu na mbichi kuhusu uhusiano wao.