Devil Worship? Makachero wamtaka Boni Khalwale kufafanua madai baada ya maafa katika shule ya Kakamega .

kk pr (1)
kk pr (1)
  Wazazi katika shule ya msingi ya kakamega  ambao wanao 15 waliaga dunia  baada ya tukio la mkanyagano watangoja kwa muda kabla ya kufahamu  kilichosababisha vifo vya watoto wao  wiki mbili zilizopita . watoto hao tayari wamezikwa lakini polisi  wanaendelea na uchunguzi ili kujua kilichotokea siku hiyo .  Shule hiyo ilifunguliwa tarehe 10 februari baada ya kufungwa kwa wiki moja . sababu kadhaa zimetolewa ili kueleza kilichofanyika siku hiyo  lakini hakuna   iliyothibitishwa kuwa halisi iliyowafanya watoto hao kukimbia na kuanguka wakitoka katika madarasa yaliokuwa katika jengo la gorofa .

Sababu hizo ni pamoja na ripoti kwamba watoto hao walishtuliwa , kuwepo imani ya kuabudu mashetani na kwamba mwalimu mmoja alikuwa na kiboko akitaka kuwachapa watoto hao . Makachero hasa wanamtaka Seneta wa zamani wa kakamega Bony Khalwale kutoa maelezo kuhusu madai yake kwamba kuna madhehebu ya kuabudu  mashetani shuleni humo .

Akizungumza na walimu ,wazazi na wanafunzi wa shule hiyo tarehe 4 Fberuari,Khalwale alizua maswali kuhusu  imani za baadhi ya makanisa ambayo hufanya maombi shuleni humo siku za jumapili . Mkuu wa  DCI katika eneo la magharibi  Shem Nyamboki amesema pindi uchunguzi wao utakapokamilishwa ,watawasilisha faili ya mapendekezo yao kwa afisi ya DPP kwa hatua zaidi kuchukuliwa .