Ajabu;Nina mume lakini nampenda mume mwingine ambaye ana mke

cheating-married-696x418
cheating-married-696x418
Ndoa na kuchumbiana kwa wakati huu sio kama ndoa za zamani zilizopewa heshima na hata kufuata utamaduni wa jamii yao.

Mwananmke mmoja aliandikia mshauri mmoja shida yake, alisema kuwa ana mume lakini hana mapenzi yake bali anampenda mwanaume mwingine cha kushangaza nikuwa mwanaume huyo ana familia yake.

Alikiri na kusema;

"Ninampenda mume wa mtu, na kila siku tunazidi kujuana zaidi na zaidi, sisi wote tuna familia zetu lakini kila siku lazima tukutane tupeane busu lakini hatujawahi shiriki ngoni nitafanya nini?" Alieleza.

Haya ndio majibu ambayo mshauri huyo alimpa baada ya kuchukizwa na jambo hilo.

Hmm unapaswa kufanya nini? nmepatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu tayari mshaanza mahusiano yenu, na kisha wahitaji ushauri, kwa hakika hautaji ushauri kutoka kwangu kwa maana unataka nikuunge mkono katika uhusiano wenu.

Unamtaka mtu akwambie kitendo ambacho unafanya ni sawa, bali si sawa unafanya ili kuumiza hisia za watu wengine, nenda ukatafute mwingine kwa sababu si mimi.

Baadaye utavuna kile ulichopanda katika uhusiano wenu, endapo familia zenu zitajuwa mnacho endeleza kinyume chao.

Kabla ya kuendelea na uhusiano wenu, fikiria hatari ambayo mnajieka nyinyi wenyewe, na pia unapaswa kufikiria jinsi ya kumwambia mume wako ili utoke katika ndoa.

Hata nasikia msisimko ukipanda kutoka miguuni hadi kichwani kwa sabau ya kitendo hicho.

Fikiria kuwa nyinyi mnakimbia katika majukumu ya familia zenu, kwa hivyo wachana na uhusiano huo kama hutaki matokeo yake yahadhiri familia zenu.

Je uko tayari kuacha familia yako kwa sababu ya upendo wa mtu mwingine au familia yako ,una hakika iko sawa au ina msukosuko wowote?