Wakali 10: Wasanii wazito wanaotesa Mombasa

Wasanii wengi wanaoshikilia hadhi ya burudani ya humu nchini huku muziki wao ukiskizwa nchini kote, Afrika mashariki na hadi ulaya.

Baadhi ya wasanii hawa wanatambulika kwa ubabe wao kuanzia zama zile kwa mfano Nyota Ndogo na Cannibal, ila sio wengi wanaojua wasanii wa kizazi kipya.

Wasanii hawa wametuwezesha kushindana na wasanii wa Bongo huku baadhi yao wakijizolea tuzo chungu nzima.

Nyota ndogo

Kwa miongo kadhaa, Nyota Ndogo amekuwa akitesa kimziki na baadhi ya nyimbo anazatambulika nazo ni 'Nibebe' akimshirikisha Nonini pamoja na 'Watu na viatu'.

Susumila

Msanii huyu mwenye sauti nzito amekuwa akipeperusha bendera ya pwani kwa mda sasa na juzi alionesha ubabe wake kwa kumshirikisha Mbosso, kwa ngoma iitwayo 'Sonona'

Otile Brown

Akiwa miongoni mwa wasanii nguli wa kizazi kipya, Otile alianza mbali na sasa hivi amejizolea mashabiki Afrika Mashariki nzima kwa nyimbo zake za mapenzi

Sudi Boy

Kama Otile Brown, Sudi ameweza kujijengea jina kote nchini huku mtindo wake wa muziki ukiwa wa mapenzi.

Cannibal

Ingawa amekuwa kimya kwa mda sasa, Cannibal ambaye huimba mitindo ya Hiphop ni miongoni mwa wasanii mashuhuri zaidi waliofungulia wengine mlango wa ufanisi.

Idd Aziz`

Idd Aziz alichipuka hivi majuzi na wimbo uliomueka kwenye darubini ya wengi ni wa 'come dada' aliomshirikisha Khaligraph Jones.

Masauti

Brown Mauzo

Wasanii wengi ni kama: Kelechi, Chikuze, Dazla na Amileena.