Tanasha hakuwa na mapenzi dhabiti kwa Diamond asema Tunda

Mmmmh nini kiini cha Tanasha na Diamond kutemana baada ya kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa miezi kumi na nne? Ni uvumi ambao umeenea sana katika mitandao ya kijamii.

Kupitia mahojiano na Bongo Tosh, tunda wa katibu la umbeya alieleza kinagaubaga kwa nini Tanasha alidai anampenda Diamond na mienendo yake ya kukaa katika uhusiano wa kimapenzi na Simba.

" Kama kuna kitu ambacho watu hawajui ni kuwa Tanasha hakuwa na mapenzi yoyote na hakuwa tayari kusema kuwa anampenda Simba na atakuwa mume wake

Alienda tu kwa malengo ya kufanikisha uimbaji wake." Tunda Alisema.

Hisia mbalimbali zimetolewa kuhusiana na kutengana kwa Diamond na Tanasha huku wengi wakiuliza ataenda nchi gani baada ya Tanasha kumuacha.

Wengi waliuliza ni mwanamke yupi atakeyekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Diamond, kwa kweli wana ngoja kwa hamu.

Tunda aliendelea na kusema kuwa Mama Dangote anataka tu kulicho chema katika maisha ya mwanawe. Awali, Tanasha alikuwa anataka kumuacha mwanawe na kurudi kwenye muziki.

Tunda alikuwa na haya ya kunena.

"Mama wa mtu ni mama hata akisema wala kutenda nini, kwa maana ameenda na mtoto wake tunachotarajia sasa ni kuwa anataka Diamond ampe msaada wa mtoto kama vile wale wengine." Aliongea.

Hakutia kikomo bali alikuwa na haya ya kusema baada ya Tanasha, kumpa block dadake Diamond katika mtandao wa kijamii wa instagram hata kumpa mama Dangote block hilo.

"Watu ambao walikuwa wanamshauri kuwa hili ama lile si zuri, alijihisi kuwa wanamzuia kufanya misheni yake." Tunda aliongea.

Je jambo hili linaweza kufika kilele kweli?