Smiling again! Mkewe Willis Raburu arejea kwa tabasamu baada ya maombolezi

Mkewe mtangazi wa runinga Willis Raburu  Marya Prude   amekuwa akipitia wakati mgumu hasa baada ya kumpoteza mwanao kabla ya kuzalwa katikamkesha wa mwaka mpya mwaka jana .

Hali imekuwa ngumu kwake huku mitandao ya kijamii ikimkosesha muda wa kuweza kuomboleza kwa amani na hata  wakati Fulani alifichua kuchoka na maisha .

Marya  wakati mmoja pia alisema alikuwa amekosa imani na mola .Wengi walimkashifu kwa kauli yake hiyo na kufanya hali kuwa mbaya hata zaidi .

Jana Prude aliweka mtandaoni picha yake akitanasamu ,shabiki wake mmoja Esther aligundua kwamba  alikuwa amereja  kwa tabasamu  na kusema chini ya picha hiyo

She is smiling again….ahsante Jehovah!

Marya Prude alijibu akisema

@esther.kalekye Yes,I’m back

Esther  aliendelea na kuandika

“@maryaprude Amen let nothing steal that joy away from you. These too shall pass. Ahsante Mungu!”

Mashabiki wake walifurahi kumuona akiwa amerejea kwa uchangamfu  na wakamhimiza adumishe furaha yake .

Willis na mkewe  walmpoteza mtoto wao Baby Adana  disemba tarehe 31 mwaka wa 2019 .Ni Willis ndiye aliyetoa habari hizo kupitia instagram