Kiingereza balaa, matusi namba one! Sudi amtaka Raila aende Nigeria kuleta dawa ya Corona

pjimage (6)
pjimage (6)
NA NICKSON TOSI

Mbunge wa Eneobunge la Kapsabet Oscar Sudi sasa anadai kuwa ni sharti kinara wa chama cha ODM Raila Odinga aende Nigeria kwa waganga wenzake alete dawa ya kuponya virusi vya Corona ambavyo vimekita mizizi katika baadhi ya mataifa ya Afrika.

Sudi ambaye kila mara amekuwa akitofautiana na Raila, amenukuliwa akisema kuwa kinara huyo wa ODM amekuwa akifanya ziara katika taifa la Nigeria, kwenda kutafuta dawa za ushirikina ambazo zitamfanya kuwa maarufu kisiasa.

Huu ndio wakate ambao Raila anastahili kusafiri kumuona daktari wake wa miti shamba ili ampatie dawa itakayotusaidia sisi kuponya hii Corona. Alisema Sudi.

Wakati uo huo Sudi amewataka wakenya kuimarisha usafi akisema ndio njia ya kipekee ambayo itapunguza virusi hivyo kutosambaa zaidi nchini.

Wakati huo Sudi amewataka wanahabari kuendelea kuhamasisha wakenya kuhusiana na Corona na si wakati wa kueneza propaganda ambazo zinapania kuligawanya taifa.

Wizara ya afya iliwashauri wakenya kuendelea kuimarisha usafi wa mikono yao na kujitenga na maeneo ambayo yamejaa watu kama njia ya kujiepusha kuambukizwa na virusi hivyo.