Polisi siku ya jumapili walipata ugumu wa kuwazuia Wakiristo nyumbani mjini Mombasa huku kaunti za pwani zikizidisha juhudi za kukabilianba na virusi vya Corona .
Maelfu ya waumini waliwasili katika makanisa mbali mbali kwa misa za jumapili bila kujali kuhusu agizo la serikali kuwataka watu kuepuka maeneo yenye umati . Baadhi ya makanisa tayari yalikuwa yamefanya misa ya kwanza mwendo wa wa saa kumi na mbili unusu alfajiri .
Vikosi vya maafisa wa usalama viliwasili katika kaisa la Jesus Celebration Centre huko Bamburi na kanisa la katoliki la Holy Ghost Cathedral katikati mwa jiji kuwatawanya watu . Katika kanisa la JCC Buxton, misa ya kwanza kati ya 6.30am na 8.30am ilifanyika kama kawaida .Polisi waliikatiza misa ya pili kuanzia saa mbili unusu asubuhi hadi saa tatu unusu .