Wachezaji wa Arsenal kusalia nyumbani licha ya mkufunzi Mikel Arteta kupona

NA NICKSON TOSI

Usimamizi wa klabu ya Arsenali umewataka wachezaji wa klabu hiyo kusalia nyumbani licha ya mkufunzi wao Mikel Arteta  kupona baada ya kuwa chini ya uangalizi kutokana na virusi vya Corona.

Taarifa za awali zilikuwa zimedai kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na baadhi ya maafisa wa kiufundi walikuwa wanatarajiwa kurejelea mazoezi yao jumanne 14 mwaka huu.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya serikali ya Uingereza kutaka klabu zote katika taifa hilo kusitisha shughuli za mazoezi kama njia ya kukabiliana na Corona .

Klabu zingine zimedinda kuwarudisha wachezaji wao kwenye kambi baada ya virusi vya Corona kuathiri maeneo kadhaa ya miji ya Uingereza .

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ndiye aliyekuwa wakwanza kuambukizwa virusi hivyo,hatua iliyofanya shirikisho la Soka Uingereza FA kufutilia mbali mitanange kadhaa ili kupunguza virusi hivyo kuenea zaidi kwa wachezaji wengine.