'Tutakutana tena’ Kipusa Mjane amkumbuka mume wake Bilionea Reginald Mengi

Jacqueline Mengi   mke wa marehemu  Reginald Mengi Bilionea wa Tanzania  ameweka ujumbe mtandaoni akieleza huzuni  na anavyomkumbuka mumewe aliyeaga dunia mwaka jana akiwa likizoni Dubai .

Jacqueline  ambaye alikuwa mshindi wa MiSS Tanzania 2000 aliiweka picha ya harusi yao  na kuandika ;

 “I hope we meet again and get a chance to love each other as we did in this life. Forever in my heart ”

  Baada ya kifo cha mume wake  Jacqueline  alipelekwa kortini na kaka mdogo wa Mengi kuhusu  urithi wa mali yake

Katika mahojiano ya hapo awali na  MillardAyo, Jacqueline  alisema shemeji yake huyo Benjamin ndiye aliyewaagiza walinzi kumzuia asifike kulitazama kaburi la mume wake .

 “I went with my kids to lay flowers on my husband’s grave. The guard stopped me and said that he had been instructed by benjamin not to let me in, unless he gives me permission.”

Anasema jambo hilo lilimkwaza sana na watoto wake walianza kulia waliposikia kilichofanyika . Alieleza kwamba mume wake alizikwa katika sehemu ambayo hakutaka .

 “Even when my husband died, we had misunderstandings on where to bury him. He had said that he should be buried in his property but his younger brother, Benjamin and his old kids (with ex-wife) refused.”

Kesi hiyo ingali mahakamani  huku mzozo kuhusu umiliki wa mali ya Mengi ukiendelea kati ya  Jacqueline na familia ya kwanza ya marehemu Mengi