Ukaidi wa maafisa wa polisi wa Kenya. Wakenya 2 wapigwa risasi na polisi na kuwaacha na majeraha

unnamed (4)
unnamed (4)
NA NICKSON TOSI

Afisa wa polisi Kabarnet kaunti ya Baringo amewapiga wakenya 2 risasi na kuwaacha wakiwa na majeraha mabaya kwa kile kinadaiwa kuwa walikiuka amri ya serikali ya kufika kwa nyumba mida ya saa 7 jioni.

Afisa huyo aliyejulikana kama Brazilian Opicho ametiwa mbaroni, usemi ambao umethibitishwa na mkuu swa polisi Baringo ya Kati Francis Gachoki.

Bring that Phone! Maafisa wa polisi wamtaka Eko Dydda kupeana Simu

Gachoki amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa wa kuabini ni nini kilichojiri hadi afisa huyo akatekeleza kitendo hicho.

Waathiriwa walikuwa mhudumu wa bodaboda  Amos Komen, 24, na muuzaji wa nguo Kabarnet Edwin Kibet, 32.

Afariki baada ya kukimbizwa na polisi kwa kukosa maski -Kibwezi

Komen alipigwa risasi kwenye kiwiko cha mkono naye mwathiriwa wa pili Kibet akakatwa mkono baada ya risasi hiyo kuupasua na kulazimu maktari kukata vidole vitatu.
Watimuliwa kama burukenge na polisi! Wabunge wanaoshabikia naibu rais watawanywa na polisi
Maafisa 2 wa polisi ni miongoni mwa watu 15 waliotiwa mbaroni wakinywa mnazi Kaunti ya Kilifi
Gachiko amesema kuwa Opicho alikuwa ameletwa kwa kituo hicho akitokea kaunti ya Nakuru alikokuwa anahudumu.