Upendo bado upo! Zari ajirekodi akisikiza wimbo wa Diamond wa Jeje

Zari Hassan aliyekuwa mpenzi wake staa wa bongo Diamond Platnumz ameonyesha na kuthibitishia mashabiki wake kuwa bado anamjali Diamond licha ya wao kutengana na kutemana.

Zari bado anafurahia kusikiza nyimbo za Diamond, hii ni baaada ya kurekodi video akiskiza wimbo wa Diamond ambao unafahamika kama Jeje.

https://www.instagram.com/p/B_0JLD4g2ri/

Akisikiza wimbo huo, Zari alikuwa anawakashifu wananchi wengi wa Afrika kusini kwa kuchukulia janga la corona kama virusi vya kawaida licha ya watu kuendelea kuambukizwa na hata wengine kupoteza maisha yao.

Awali Zari alikuwa amemuita Diamond deadbeat father kwa kutojua wanachokula watoto wake.Baada ya Diamond kuitwa majina hayo alifanya hatua moja na kuwapigia simu wanawe, kwa muda huo wote wawili hao wamekuwa wakizungumza au kujuliana hali kupitia kwa mawakili wao.

Akiwa katika mahojiano na runinga ya Wasafi, Diamond alijibu madai hayo na kisha kusema ana matumaini virusi vya corona vikipungua wataweza kuwalea watoto wao ipasavyo na si kama awali.

Alisema thamani ya Zari katika macho yake haitawahi kubadilika.