Mulamwah, Je wajua kwamba mcheshi huyu ni muunguzi?

David Oyando almaarufu Mulamwah amewacha mashabiki wake vinywa wazi baada ya kufichua kwamba aliacha taaluma ya uuguzi na kuanza ucheshi.

Mulamwah alisema kuwa alijaribu sanaa ya ucheshi akiwa katika mafunzo ya nyanjani katika hospitali kuu ya Kenyatta.

"Nilifanya video yangu ya kwanza nikiwa kwenye mafunzo ya nyanjani  katika hospitali kuu ya Kenyatta, mimi ni muuguzi na nimehitimu katika taaluma hiyo." Mulamwah Alizungumza.

Mcheshi huyo alifichua kuwa alisomea uuguzi katika chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret na kisha kuhitimu mwaka wa 2018.

"I studied a degree in nursing at Moi University in Eldoret and graduated in 2018. I repeated a few times but I finally managed to pass and graduated." Aliongea.

Mulamwah alifichua kuwa alisomea uuguzi kumfurahisha tu babake aliyekuwa akimshinikiza aisomee.

Kulingana na mcheshi huyo, baba yake hakucheza na masomo na alitaka wasome kwa bidii.

"Between nursing and comedy, you will see that I am more inclined to the latter. We want to school because of dad's pressure. He wanted us to get to school, study and graduate. I really hated doing that but I had to and I struggled with nursing a very tough course." Alieleza.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO